
FUKARA MWENYE BUSARA
Je, Thamani ya Binadamu Inapimwa kwa Mfuko au kwa Akili?
Katika kijiji cha Masononeko, umaskini si hali tu ya kukosa mali—ni kilema kinachokufanya uonekane mnyama mbele ya wenye ukwasi. Jackson, kijana anayeishi kwenye banda la matope na kuvaa mavazi yenye viraka, anaitwa "Fukara Pumbavu" na walevi wa kijijini kwa sababu ya ukimya wake na unyenyekevu.
Lakini ndani ya moyo wa Jackson mna siri kubwa: busara iliyopitiliza na imani thabiti kwa Rabuka. Wakati matajiri wakimfukuza kama mbwa koko na kumpa makombo ya vyakula, Jackson anasubiri muujiza ambao umeanza kutokota mbinguni.
"Fukara Mwenye Busara" ni kisa kinachochambua mpaka uliopo kati ya fukara na tajiri, kikitupeleka hadi katika "Ikulu ya Kifo" ambapo kila mmoja ni sawa. Je, busara ya Jackson itamtoa kwenye ziwa la ufukara, au jamii itaendelea kumzika akiwa hai katika dharau za wakwasi?
Customer Reviews
Write a Review
Click here to rate this book.
No reviews yet. Be the first verified purchaser to share your thoughts!